‘PANDE’ mojawapo kati ya zile mbili zinazopigania ‘madaraka’ katika klabu ya Stand United ya Shinyanga inakaribia kufikia uamuzi wa kikatiba kisha kuiondoa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo katika michuano.
Uamuzi huo unataraji kufikiwa na upande ambao ulienguliwa na Shirikisho la soka nchini-TFF. Tayari Stand imecheza game moja katika VPL msimu huu (Stand United 0-0 Mbao FC.)
“Watu wawili/watatu pembeni walikuja kwangu. Nilisikia wanakwenda Ikulu. Nikawaambia, ‘nendeni halafu mtarudi. Mimi ndiye Waziri wa michezo, halafu Waziri mjanja. Hamuwezi mkanizunguka.”
“Wakarudi, waliporudi nikawaambia, ushauri wangu nendeni mkakae mezani, nyinyi mliogomea (upande unaotaka kuiondoa timu katika ligi ambao uligomea uchaguzi uliopita) na wale waliochaguliwa halafu mmalize tofauti, wala hakuna shida katika hili. Hii ya kumaliza tofauti ni upendeleo kwao, kwa sababu wao ndiyo waligomea uchaguzi wakijua wataanguka,” anasema waziri, Nape Nnauye kuhusiana na mgogoro huo wa timu ya Stand United.
“Sasa mimi ushauri wangu ni kwamba, waende wakakae mezani. Wamemtukana sana Mkuu wa Wilaya, wamenitukana sana mimi kwenye simu. Wamefanya mambo mengi sana, lakini sasa mtoto wako hata akipiga kelele sana, unamsamehe tu. Nadhani wamejifunza.”
“Kikubwa hapa, waende wakakae wazungumze waone namna ya kumaliza tofauti zao kwa sababu mwisho wa siku wasipomaliza watawafukuzu wadhamini wao na kile wanachokigombania kitaondoka.”
“Na kwa kweli ACACIA (wadhamini wa Stand) wameonesha interest ya kujiondoa kwa sababu itawachafua. Sasa wakishaondoka mlichokuwa mnakipigania mnakikosa na timu yote mnaikosa. Kwa hiyo hizi kelele, waziri sema, waziri sema, hili litamalizwa na wenyewe. ‘Mwiba ulipoingilia ndipo unapotokea’ kwa nini mnataka muutolee sehemu nyingine?” anasema waziri, Nape.
No comments:
Post a Comment