SIMBA SPORTS CLUB
DAR ES SALAAM
29-6-2016
Klabu ya Simba inayo furaha kubwa ya kutangaza kumshukuru mlezi wake bwana Mohammed Dewji kwa kuanza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo.
Dewji maarufu kama MO tayari ameshaanza kulipia mishahara ya wachezaji,benchi la ufundi na Sekretarieti ya klabu na atafanya hivyo katika kipindi chote cha mpito kuelekea mabadiliko ya kimuundo ya klabu.
Mbali ya hayo mfanyabiashara huyo mkubwa barani Afrika atalipia kodi za nyasi bandia na gharama nyingine za uendeshaji wa klabu.
Uongozi wa Simba unamshukuru sana MO,ukizingatia klabu kwa sasa haina mdhamini na unaamini uwekezaji huo ni chachu ya kuwarejeshea furaha wanasimba na hatimae kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya msimu huu na misimu mingi ijayo.
Mwisho klabu inawaomba washabiki wake wajitokeze kwa wingi siku ya Jmosi ya Octoba Mosi pale uwanja wa Taifa,kuishangilia Timu yao itakapocheza mechi ya ligi dhidi ya Yanga.
Tunaamini mechi hiyo ni mwendelezo wa furaha kwa wanachama na washabiki wetu kote nchini.
Pia tuwaombe sana kukumbuka kununua tiketi kwa mawakala wa Selcom waliopo katika maeneo mbalimbali.
Ikumbukwe tiketi za mechi hii ni za kieletroniki.
Imetolewa na
HAJI S.MANARA.
MKUU WA HABARI
SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA
No comments:
Post a Comment