Laudity Mavungo huenda ikaota mbao baada ya juzi kukutwa uwanja wa ndege wa nchi burundi kwenda nchini Ufaransa kwa ajili ya majaribio katika klabu ya Tours inayoshiriki ligi daraja la pili.
Simba ambayo iliingia mkataba na straika huyo mwaka jana ambapo alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na vital'O iliyohitaji dau kubwa ili kumuachia mchezaji huyo kujiunga Simba.
Taarifa za uhakika zilizoifikia jijini jana kutoka kwa rafiki wa karibu wa Mavugo kwamba mchezaji huyo amepata dili Ufaransa na juzi (jumamosi) kwenda nchini humo kwa majaribio.
Alisema siku hiyo alikutana na mchezaji huyo uwanja wa ndege akiwa na familia yake ikimuaga kwa ajili ya safari ya kuelekea nchini humo.
"Nilikutana nae uwanja wa ndege wa Burundi, akiwa na familia yake wakimuanga kwani amepata ofa ya kwenda ufransa kufanya majaribio katika timu ya Tours inayoshiriki ligi daraja la pili," alisema rafiki huyo.
Alisema endapo Mavugo akifuzu katika majaribio hayo huenda asijiunge tena na Simba wala Vital' O na kusaini mkataba katika timu hiyo.
@@@@@
No comments:
Post a Comment