KOCHA wa timu ya Yanga Mholanzi Hans Van Pluijm hajakata tamaa na naona kuna uwezekano mkubwa wa kikosi chake kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Yanga ipo katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho jana aliamvulia pointi 1 katika michezo aliyocheza ambapo jana alilazimishwa sare ya bao 1-1, mchezo uliochezwa uwanja wa taifa.
Mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara hawana nafasi baada ya kijikusanyia alama moja huku wakiwa na michezo miwili ugenini na mmoja nyumbani dhidi ya Mo Bejaia ambao waliwafunga katika mchezo wa awali.
Pluijm alisema vijana wake walicheza vizuri lakini tatizo la kutokutumia nafasi wanazopata linaendelea kuwaandama.
"Tunaweza kufuzu katika hatua ya nusu fainali , kwakua katika mpira kila kitu kinawezekana,tumebakiwa na mechi tatu na tukishinda zote tutakuwa na alama kumi," alisema.
Hans alisema hajakata tamaa akiamini mechi zilizobakia ikiwa moja ya nyumbani na ugenini kufanikiwa kushinda.
Alisema baada ya mchezo wao dhidi ya medeama wanaenda kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo huo na kujiimarisha katika michezo iliyobakia ya kundi hilo.
No comments:
Post a Comment