Friday, July 29, 2016

MWADINI,KIMWAGA WATOLEWA KWA MKOPO AZAM FC


UONGOZI wa klabu ya Azam FC, umeweka wazi kuwatoa wachezaji wake wanne kwa mkopo ambao ni  Mwadini Ali, Ame Ali ‘Zungu’ Abdallah Khery na Joseph Kimwaga.

Akizungumza na Jambo Leo, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Idrissa Nassor, alisema kuwa wachezaji hao ambao bado wana mikataba katika klabu yao, wameamua kuwapa nafasi za kucheza kupitia klabu za African Lyon, Simba na Mwadui FC.

Nassor alisema Mwadin Ali na Ame Ali wataichezea Simba, kwa sasa wanaendelea kufuata utaratibu wa uhamisho huo wa mkopo, Kimwaga ataitumikia klabu ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga na Kheri ataichezea klabu ya African Lyon.

Alisema kwa upande wa Mwadin na Ame wakati wowote kuanzia Jumatatu watajiunga na klabu ya Simba kwa kuwa vitu vilivyobaki kukamilisha uhamisho huo ni vidogo.

“Mwadini na Ame, Kimwaga na Kheri  wote tumewatoa kwa mkopo, lakini wakifanya vizuri katika klabu hizo hata kwenye mzunguko wa pili wa msimuu ujaoanza wanaweza kurejea katika klabi yetu, kikubwa ni kocha kiridhika na uwezo wao ambao itauonesha"alisema Nassor.

Alisema klabu hiyo katika msimu uliopita ilimtoa kwa mkopo mchezaji wake kwa mkopo  katika klabu ya Mwadui na mwaka huu mchezaji huyo amerejea katika kikosi cha Azam na anaitumikia.

Wakati huo huo klabu ya Azam FC leo itajitupa kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar kuvaana na timu ya Jang'ombe, mchezo wa kirafiki wa kijipima nguvu ikiwa sehemu ya kujiandaa na mchezo wa ngao ya jamii utakaofanyika Agosti 17 dhidi ya Yanga.

Nassor alisema kuwa mchezo huo utacheza saa 2.usiku ambapo utakuwa ni mchezo wa pili baada ya kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya kombaini ya Zanzibar,


No comments:

Post a Comment