Mfanyabishara
kijana na maarufu ndani na nje ya nchi, Mohammed Dewji ‘MO’ ambaye
ametajwa kutaka kuwekeza kwenye Klabu ya Simba kwa kutoa Sh bilioni 20,
jana aliibuka kwenye mchezo wa kirafiki wa timu hiyo dhidi ya Moro Kids.
Katika
mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia Highlands,
Morogoro uliishuhudia Simba ikishinda mabao 2-0 dhidi ya wenyeji hao na
kuwa ushindi wa pili mfululizo baada ya wiki iliyopita kuifunga Polisi
Moro mabao 6-0.
Mabao
ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajib dakika ya 20 akipokea pasi ya Shiza
Kichuya na la pili lilifungwa na Danny Lyanga dakika ya 69 akiunganisha
pasi ya Mohammed Ibrahim.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, mashabiki waliojitokeza uwanjani hapa muda
wote wa mchezo walikuwa wakiimba nyimbo za kuushinikiza uongozi umpe
timu MO.
Mashabiki hao walisikika wakiimba: “Mo tumpe timu.”
Baada ya mchezo huo Kocha Joseph Omog wa Simba alisema, amefurahishwa na uwezo ulioonyesha na wachezaji wake huku akidai wapinzania wao walikuwa katika kiwango bora zaidi
No comments:
Post a Comment