Wednesday, July 27, 2016

MWAKALEBELA CUP KUANZA SIKU ZA USONI

DIWANI wa Kata ya Wazo,  Mh .Joel Mwakalebela  amezitaka timu zote zilizopo katika Kata yake kujitokeza kwa wingi kuweza kushiriki katika mashindano ya Mwakalebela CUP yanayotarajiwa kuanza mwezi wa Septemba.

Akizungumza jana  Joel Mwakalebela alisema kuwa mitaa nane itashirikia katika mashindano hayon na  lengo  ya kuanzisha mashindano hayo ni  kwaajili ya kusaka vipaji na kukuza soka.

"Vijana wengi wanavipaji ila wanakosa wadhamini wa kuwaendeleza katika soka hivyo nimeamua kuanzisha mashindano hayo kwa lengo la kusaka vipaji kwa  vijana, kama tunavyojua soka ni  ajira naomba vijana kujitokeza kwa ajili ya kushiriki katika mashindano haya ili kupata timu bora katika Kata yangu"alisema.

Aliongeza kuwa katika mashindano hayo yatasimamiwa pia na mtaalam wa soka ambae ataangalia vipaji vya soka ili kuweza kupata vipaji vya soka katika Kata ya Wazo.

Alifafanua kuwa mashindano hayo yanatarajia kutoa timu moja kwa ajili ya Kata ya Wazo ambayo itashiriki katika mashindano ya soka na kuwakilisha kata ya wazo.



No comments:

Post a Comment