Friday, July 29, 2016

TCHETCHE AZIKANA SIMBA,YANGA

MBULIAJI wa Azam FC, Kipre Tchetche amesema hajawahi kufanya mazungumzo na klabu kongwe hapa nchini za Simba na Yanga kwa ajili ya kuzitumikia timu hizo kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kipre ambaye yuko nchini kwao na huku pacha wake Michael Bolou tayari amejiunga na kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa na Ligi hiyo pamoja na michuano ya kimataifa (CAF) mwakani.
Kuna tetesi kwamba mchezaji huyo amegoma kurejea nchini huku akihitaji uongozi wa Azam kumruhusu ili ajiunge na mmoja ya timu hizo mbili Simba au Yanga.
Akizungumzia sakata hilo, Kipre aliyekuwa nchi kwao Ivory Coast, alisema hana mpango wa kucheza soka Tanzania hivyo hakuna ukweli  suala la kufanya mazungumzo Simba au Yanga.
Alisema hayo maneno amekuwa akizushiwa tangu msimu uliopita ambapo walianza kumuhusisha na Yanga ambapo kwa sasa Simba jambo ambalo halinaukweli.
“Hayo maneno sio ya kweli kabisa kwa sasa sijafikiria kucheza soka Tanzania, nahitaji kupata changamoto za soka nchi zingine mbali na Tanzania kwani nimekaa na kucheza soka zaidi ya miaka mitatu ,” alisema.
Kipre ambaye bado yuko nchini kwao licha ya pacha wake Michael Boluo kujiunga na timu hiyo iiliyopo kambini kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu pamoja na michuano ya kimataifa (CAF) mwakani.
Alisema hadi sasa hajakuwa na maamuzi sahihi zaidi ya kuisubiri viongozi wake kuweza kumpa ruhusa hiyo ya kumuondoa katika kikosi chao kwa msimu ujao.
“Suala la lini nitakuja huko bado sijajua kwani viongozi hawajaonyesha nia yoyote ya kuniondoa jina langu katika orodha ya wachezaji wao msimu ujao, hivyo ka

No comments:

Post a Comment