Friday, August 5, 2016

AJENDA ZA MKUTANO MKUU YANGA HADHARANI

NGOZI wa klabu ya Yanga umetangaza ajenda zitakazo jadiliwa kesho kwenye mkutano mkuu wa dharura utakaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa 3 asubuhi.

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari Meneja masoko na mratibu wa matawi wa klabu hiyo Omari Kaya amewataka wanachama wengi kujitokeza kwa wingi ili maamuzi yatakayotolewa yawe yameridhiwa wanayanga wote ili kuondoa malalamiko ambayo hayana msingi.

"Tunaomba wanachama wetu wajitokeze kwa wingi ili tujadili masuala mbali mbali yanayoihusu klabu yetu ya Yanga," alisema Kaya.

Kaya aliziainisha ajenda hizo kama ifuatavyo:
1.Tathimini ya mashindano klabu ya Yanga iliyoshiriki kwa mwaka huu.
2.Ushirikiano uliopo baina ya Shirikisho la mpira wa miguu TFF na Yanga.
3.Marekebisho ya Katiba.
4.Mapato na matumizi.
5.Shukrani kwa viongozi waliomaliza muda wao.
6.Maendeleo ya klabu.
7.Mengineyo.

Aidha Kaya alisema pia endapo wanachama wataridhia kubadili uendeshwaji wa klabu hiyo kama walivyofanya watani wao Simba uongozi hautasita kulifanyia kazi suala hilo kwakua litakuwa na manufaa kwa Yanga.

Pamoja na mkutano huo kesho kikosi cha Yanga kitashuka dimbani kucheza na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa kirafiki utakaofanyika uwanja wa Taifa saa 10 jioni huku kiingilio kikiwa ni shilingi 5,000 kwa majukwaa yote

No comments:

Post a Comment