Mkuu wa
Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Jerry Muro amesema
kuwa ataendelea na majukumu yake kama kawaida mpaka atapopelekewa nakala
ya hukumu toka Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.
Julai 7 mwaka huu Kamati
ya maadili ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Wakili msomi Wilson Ogunde
ilimfungia Jerry kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na
faini ya shilingi milioni moja baada ya kukutwa na makosa matatu ya
kimaadili.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mitaa ya Twiga na Jangwani
jijini Dar es Salaam Jerry alisema amepokea barua ya kusimamishwa kazi
ila bado hakupewa nakala ya hukumu kwahiyo haimzuii kuendelea na
majukumu yake ndani ya Yanga.
"Nilikuwa likizo,
nimeripoti kazini Agosti mosi kuendelea na majukumu yangu kama Ofisa
Habari wa klabu ya Yanga huku nikisubiri nakala ya hukumu toka TFF
itakayonipa mwanga wa kitu cha kufanya kwa sasa naendelea na kazi kama
kawaida," alisema Jerry.
Aidha Jerry alisema pia
atakapota nakala hiyo ataangalia uwezekano wa kukata rufaa huku akifuata
maagizo toka kwa mwajiri wake klabu ya Yanga wa kitu gani cha kufanya.
" Kuna mambo mawili nitakayofanya kama kukata rufaa au kusikiliza mwajiri wangu anataka nini," alisema Jerry.
No comments:
Post a Comment