Sunday, August 7, 2016

KUELEKEA MAN UNITED DHIDI YA LEICESTER CITY LEO HII

bingwa watetezi wa Ligi Kuu England Leicester City leo wana kibarua kizito pale watakapokuwa wakichuana na Mabingwa Watetezi wa Kombe la FA Manchester United kwenye mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii utakaochezwa kunako dimba la Wembley majira ya saa 12 za Afrika Mashariki.
Mchezo huu unavuta hisia za wengi kutokana ubora walioonesha Leicester msimu uliopita na ubora wa kikosi cha Man United cha sasa chini ya utawala mpya wa kocha Mreno Jose Mourinho.
Kocha wa Leicester Claudio Ranieri anasema kwamba, ameshasahau ubingwa waliochukua msimu uliopita na kuelekeza nguvu zake kwenye msimu mpya unaofunguliwa rasmi baada ya mchezo wa leo.
Kocha wa Man United Jose Mourinho anasema kwamba, mchezo huu una maana kubwa sana kwa hasa kwa wachezaji wake ambao walikuwa sehemu ya timu iliyobeba ubingwa wa FA msimu uliopita.
“Tunalitaka kombe hili kwa udi na uvumba lakini tunajua mchezo utakuwa mgumu sana,” Ranieri amesema.
“Nimeshasahu yote yaliyotokea msimu uliopita. Na sasa maco yangu yote nayaelekeza kwenye msimu mpya wa ligi.”
Ranieri anasema kwamba wako imara kabisa, huku mshambuliaji wao tegemezi Jamie Vardy akirejea rasmi mazoezini baada ya kutoka kuitumikia timu yake ya England kwenye Michuano ya Euro mwaka huu.
“Mameneja na wachezaji wote wanataka kucheza katika dimba la Wembley. Ni moja ya viwanja maarufu kabisa ulimwenguni,” alisema.
Huu sio mchezo wa kirafiki. Tutacheza kwa nguvu zetu zote na naamini vivyo hivyo kwa Manchester United pia. Timu zote zinataka kushinda.”
Mourinho ambaye amerithi mikoba ya Louis van Gaal wiki moja tu baada ya kubeba ndoo ya FA kufuatia kuwatwanga Crystal Palace mwezi Mei, hajawa na matokeo mazuri sana kwenye mechi za pre-season.
Mchezo dhidi ya mahasimu wao Manchester City uliotakiwa uchezwe China July 25, ulifutwa baada ya uwanja kuharibika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.
Wiki ambayo ilienda bure nchini China ilikuwa mbaya sana kwetu.” Mourinho alisema. “Hivyo tunahitaji kufanya mazoezi kwa bidii sana, tunahitaji kucheza, tunahitaji kuwapa muda wachezaji.
“Kwa sasa hatuna tena nafasi ya kufanya mazoezi dhidi ya timu nyingine (mechi za kirafiki). Tunao huu mchezo dhidi ya Leicester pekee kabla ya msimu mpya kuanza, na hata hivyo mchezo huu si sehemu ya mazoezi bali mchezo rasmi.
“Tunakiwa kucheza mchezo huu kama mechi na sio mazoezi. Tuna nafasi ya kuwapa muda muda baadhi ya wachezaji. Baadgi ambao najua hawawezi kucheza kwa dakika 90, lakini bila shaka tutajaribu kuhakikisha tunashinda mchezo huu.”
Takwimu za mechi zao walizokutana.
  • Mchezo pekee uliozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Wembley, ulikuwa ni mchezo wa fainali ya Kombe la FA mwaka 1963, ambapo Man United walishinda mabao 3-1.
  • Michezo yote miwili kati ya United na Leicester kwenye ligi ya msimu uliopita iliisha kwa sare ya bao 1-1.
  • Jamie Vardy alivunja rekodi ya Ligi ya England kwa kufunga kwenye mechi nyingi mfululizo, rekodi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Mholanzi Ruud van Nestrooy ambaye alifunga magoli 11 kwenye mechi 11.
Leicester City
  • Hii ni mara ya kwanza kwa Leicester kuwania taji la Ngao ya Jamii tangu mwaka 1971, ambapo waliifunga Liverpool bao 1-0 huko Filbert Street. Leicester walikuwa ni washindi wa Ligi Daraja la Pili (kwa sasa Championship) msimu mmoja kabla.
  • Mara ya mwisho Leicester kucheza katika Uwanja wa Wembley ilikuwa ni kwenye Kombe la Ligi mwaka 2000, ambapo walishinda mabao 2-1 dhidi ya Tranmere
  • Katika michezo mitano waliyocheza kwenye Uwanja wa Wembley, Leicester wameshinda mara tatu na kutoka sare mara moja dhidi ya Middlesbrough mwaka 1997 kwenye Kombe la Ligi, na baadaye kushinda kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa Hillsborough.
  • Hii ni mara ya kwanza kwa kocha Claudio Ranieri kushuhudia timu yake ikicheza katika Dimba la Wembley.
  • Vardy amefunga mara moja na kutoa assist moja kwenye mechi tatu za England kwenye Uwanja wa Wembley.
Manchester United
  • Hii inakuwa ni mara ya 30 kwa Manchester United kucheza Wembley kuwania taji la Ngao ya Jamii. Wameshinda taji hilo mara 20.
  • United wameshinda taji hili mara tano ndani ya sita ya mwisho waliyocheza (2007, 2008, 2010, 2011, 2013).
  • Pia wameshinda michezo minne ya mwisho waliyocheza Wembley tangu walipopoteza mwaka 2011 kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona.
  • Josem Mourinho ameshindwa kuchukua taji hili mara tatu kati ya nne akiwa kama kocha wa Chelsea, ikiwemo msimu uliopita dhidi ya Arsenal, huko mchezo mmoja akifungwa kwa penati na Man United mwaka 2007.
  • Manchester United wampoteza mchezo mmoja kati ya 15 kwenye mashindano yote dhidi ya Leicester (ushindi mara 11, droo mara 3)
  • Zlatan Ibrahimovic amewahi kuccheza mara moja tu katika Uwanja wa Wembley, wakati Sweden walipofungwa bao 1-0 na England Novemba 2011.


No comments:

Post a Comment