ROMELU LUKAKU anakaribia kurejea Chelsea kwa usajili utakaovunja rekodi ya klabu baada ya Everton kukiri kuwa ipo hatarini kumpoteza mshambuliaji huyo. Chelsea ilishuhudia ofa yao ya pauni 57 ikipigwa chini na Everton ambayo ilisema thamani ya mchezaji wake ni pauni milioni 75. Lakini kocha wa Chelsea Antonio Conte ana matumaini ya kumnasa Lukaku baada ya Everton kunukuliwa na gazeti la The Mirror ikiweka wazi kuwa mshambuliaji huyo ameomba kuondoka. Ofa ya Chelsea iliyokataliwa ni mara mbili ya bei ya pauni milioni 28 ambayo Mourinho alipokea pale alipoamua kumpiga bei mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23 mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment