Na Tausi Salum
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amekabidhi ramani ya
michoro ya Viwanja kwa Balozi wa China nchini Lu Youqing, ikiwa ni
ahadi yake ya kuboresha Viwanja Vitatu vya Mkoa wa Dar es Salaam.
Makonda amekabidhi ramani hiyo wakati wa hafla fupi ya chakula cha
usiku kwa timu tatu zilizofanya vizuri kwenye michuano ya Sports
extra ndondo cup iliyomalizika mwishoni mwa juma lililopita,
iliyofanyika jana usiku katika ubalozi wa China nchini uliyopo
Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Timu zilizoalikwa kwenye chakula hiko ni mshindi wa tatu wa
mashindano hayo Makumba FC, washindi wa pili Kauzu FC na mabingwa
wa michuano hiyo Temeke Market.
Makonda aliahidi kuboresha Viwanja vitatu , kimoja katika kila
Wilaya ya Ilala,Temeke na Kinondoni ili kulinda afya za wachezaji
na kuendelea michezo Mkoani mwake.
Akikabidhi ramani hiyo Makonda alimshukuru Balozi Lu kwa kukubali
ombi lake la kusaidia kuboresha Viwanja hivyo , kwa ajili ya
Wananchi wake.
Alisema wakati anatoa ahadi ya kuboresha viwanja hivyo hakujua ni
wapi angepata pesa, lakini kwa kuwa ana mahusiano mazuri na wadau
wa michezo na yupo karibu na watu alijuwa jambo hilo lazima
litatimia.
Akizungumzia mashindano ya sports extra ndondo cup amesema
yamekuwa msaada mkubwa katika kupunguza vitendo vya kiuhalifu na
kihuni , kwa sababu yamewahusisha Vijana wa mitaani ambao wengi
wao hawana shughuli za kufanya.
Amemshukuru Balozi huyo kwa kukubali mwaliko wake wa kwenda
kushuhudia mchezo wa fainali uliowakutanisha Kauzu FC na Temeke
katika Uwanja wa Chuo cha Utalii , ambapo Temeke walishinda kwa
mabao matatu kwa moja.
Anasema kitendo cha Balozi huyo kukubali mwaliko wa kwenda
kushuhusdia mchezo huo, kimezidi kudumisha urafiki uliyopo kati ya
nchi hizo mbili yaani Tanzania na China na kuendelea kuudumisha
zaidi.
Kwa upande wake Balozi Lu Youqing amesema kitendo cha mashabiki
wengi wa soka kujitokeza kushuhudia mchezo huo wa fainali licha ya
kiwanja kutokuwa kwenye hali nzuri ,kimeonyesha namna ambavyo
Watanzania wanavyopenda michezo hususani mchezo wa soka.
Alisema anaamini siku moja wachezaji hao wanaweza kucheza ligi ya
China ambayo imekuwa maarufu sasa hivi Duniani, na wachezaji wengi
maarufu na weusi wamekuwa wakienda kucheza.
mwisho
Na Tausi Salum
KIKOSI cha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti
Boys,kesho kinashuka kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto,
Magharibi mwa Mji wa Johannesburg, Afrika Kusini kucheza na
wenyeji katika mchezo wa awali kuwania nafasi ya kufuzu fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika, zitakazofanyika Madagascar hapo
mwakani.
Afrika Kusini ambayo Serengeti Boys inacheza nayo kesho ni mtihani
wa kwanza kati ya miwili kabla ya kutinga Madagacar. Mchezo wa
kwanza unafanyika hapa Afrika Kusini, kabla ya kurudiana Agosti
21, 2016 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi-nje kidogo ya jiji
la Dar es Salaam.
KIkosi hicho chini ya Kocha Bakari Shime, kinaingia Uwanjani
kikiwa na ari, nguvu na kujaa hamasa na matumaini ya kushinda,
timu ya mpira wa miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
‘Serengeti Boys’, kesho Jumamosi Agosti 6, 2016 itaingia Uwanja wa
“Tutaifunga Afrika Kusini hapa kwao,” ni maneno ya Mchawi Mweusi -
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, alipozungumzia mchezo huo utakaoanza
saa 9.00 alasiri kwa saa za Afrika Kusini wakati huko Tanzania
itakuwa ni saa 10.00 jioni katika uwanja ambao hutumiwa na timu ya
Moroka Swallows ambayo kwa sasa imeshuka daraja hadi la pili.
Shime amesisistiza: “Najua Afrika Kusini watataka kutumbia mbinu
za nyumbani. Lakini sina wasiwasi. Nimelenga kushinda michezo yote
iliyo mbele yangu. Si kwamba napigania kufuzu kwenda Madagascar tu
kwenye fainali za Afrika, la hasha, nataka timu hii niipeleke
Kombe la Dunia.”
Shime ambaye alianza na timu hiyo mwaka mmoja uliopita, amerudia
maneno yake: “Sioni kama itakuwa kikwazo kuifanikisha kufika
fainali za Kombe la Dunia. Namuomba Mungu atunyooshee mkono wake,
nawaombea viongozi wa TFF wazidi kuihudumia timu hii, lakini pia
wadau wengine waisapoti timu hii bila kuangalia au kuchagua mtu
anayeongoza TFF. Hii ni timu ya Watanzania wote.”
Shime alishukuru mipango na ahadi ya Rais wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kugharamia kambi ya siku 10
iliyoyofanyika Madagascar akisema: “Ilikuwsa ni kambi bora. Kwa
sasa kikosi changu kinahitaji kulipam deni la Watanzania na ahadi
ya Rais Malinzi.”
Kikosi tarajiwa leo ni Ramadhani Awm Kabwili atakayecheza golini,
Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Vitalis Nkosi,
Dickson Nickson Job, Shaban Zuberi Ada, Kelvin Nashon Naftal, Ally
Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Mohammed Abdallah Rashid
Ibrahim Abdallah Ali na Syprian Benedictor Mtesigwa.
Ili kufika hapo, Serengeti iliifunga Shelisheli jumla ya mabao 9-0
katika mechi mbili za Tanzania na Shelisheli.
Hivi karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako
walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na
FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na
rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za
Afrika Mashariki. Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na
Marekani.
No comments:
Post a Comment