Na Tausi Salum
UONGOZI wa klabu ya Simba unapenda kutoa taarifa kwa
wanachama,wapenzi wake na washabiki wa mchezo wa mpira wa miguu
kote nchini kuwa tamasha la kila mwaka la klabu yetu
linalojulikana kwa umaarufu wa Simba Day lipo pale pale na wala
'halijapeperushwa' kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya
habari nchini.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Habari wa klabu ya
Simba, Haji Manara imesema kuwa kuna upotoshaji mkubwa
usiozingatia weledi na maadili ya taaluma kulikopitiliza
kulikofanywa na chombo hicho ambao unaweza kuleta athari kubwa kwa
tamasha letu ambalo ni sehemu ya sherehe muhimu ya kuadhimisha
miaka themanini toka kuanzishwa kwa klabu yetu yenye historia ya
kutukuka ndani na nje ya mipaka yetu kupita klabu yoyote nchini.
Manara alisema kuwa katika ratiba ya tamasha letu hili kesho
kutakuwa na shughuli ya usafi kwenye mtaa wa Msimbazi yalipo makao
makuu ya klabu na shughuli hii itaanza saa mbili kamili asububi na
mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mbunge wa jimbo la Ilala yalipo
makazi ya klabu Mh Mussa Azzan Zungu.
Tunawaomba wana Simba wote mjumuike kwenye jambo hili muhimu
ambalo pia ni maagizo ya Rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania.Mh John Pombe Magufuli.
Pia hiyo kesho Jumamosi ya tarehe 6-8-2016 itakuwa ni siku ya
kupiga picha za msimu kwa wachezaji na benchi zima la ufundi la
klabu ya Simba.
Jumapili ya tarehe 7 ni siku ya wachezaji na benchi la ufundi kuwa
live mitandaoni kwa kuperuzi na wana Simba kuhusina na masuala
mbali mbali.
Sambamba na mkutano na wanahabari kati ya makocha na manahodha wa
klabu ya AFC Leopard ya Kenya na sisi wenyeji wao Simba SC.
Kilele cha sherehe zenyewe ni siku ya Jumatatu tarehe nane mwezi
No comments:
Post a Comment