Sunday, August 21, 2016

MAVUGO AFUNGUA TAWI LA SIMBA BURUNDI


August 21, 2016

NA SAADA SALIM

BAADA ya kujiunga na Simba, straika wa kimataifa wa timu hiyo, Laudit Mavugo, amekuwa gumzo nchini kwao Burundi ambapo idadi kubwa ya marafiki na ndugu zake wamekuwa wakimwomba awatumie jezi za Wekundu hao wa Msimbazi jambo linalotafsiriwa kama amefungua tawi nchini humo.

Straika huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu, ameliambia DIMBA kuwa tangu kutua hapa nchini amekuwa akipokea simu nyingi kutoka Burundi marafiki zake wakimtaka kuwatumia jezi za Simba.

“Tangu nitue hapa Tanzania marafiki zangu wengi wamekuwa wakinipigia simu niwatumie jezi za kutosha za Simba hasa namba tisa ambayo ninaitumia, wamekuwa wakinipa sapoti kubwa sana.

“Nadhani nitafanya kama wanavyotaka kwani mtu akikupa ushirikiano inatakiwa hata wewe umthamini ili kuzidi kujenga urafiki ulio imara,” alisema

No comments:

Post a Comment