Sunday, August 21, 2016

BENTEKE RASMI CRYSTAL PALACE,KLOOP AMWAGIA SIFA

Benteke alikuwa jijini London tangu jana Ijumaa kwa ajili ya vipimo vya afya ambapo baada ya kukamilisha taratibu alitambulishwa rassmi.

Usajili huo umekuja baada ya mchezaji huyo kutokuwa katika wakati mzuri kwa kushindwa kutamba Liverpool tangu alipotua akitokea Aston Villa.

Akizungumzia juu ya usajii huo, Benteke ambaye ana umri wa miaka 25 alisema: “Nina furaha kutua hapa Crystal Palace, nategemea kufanya mengi kwa kujituma.”

Benteke amefunga mabao mabao 51 katika Premier League katika misimu minne aliyocheza katika ligi hiyo.


Wakati huo huo,kocha wa timu ya Liverpool amemwagia sifa mshambuliaji huyo na kuwaambia Palace kuwa wamepata kifaa.

No comments:

Post a Comment