iki iliyopita Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, alitangaza kuendelea kupiga kazi kama kawaida na kwamba hatambui adhabu yake ya kufungiwa mwaka mmoja aliyopewa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwani hajapewa barua ya hukumu yake, hata hivyo TFF imemwambia asithubutu kwani kama ni barua ya adhabu alishakabidhiwa.
Muro, juzi Ijumaa kwenye vyombo vya habari alisema alikuwa likizo na si kutumikia kifungo hicho alichopewa baada ya kukutwa na hatia ya kupingana na maamuzi ya TFF pamoja na kutakiwa kulipa faini ya milioni tatu.
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, ameliambia amesema kuwa Muro anajua nini kitamtokea iwapo atathubutu kufanya kazi kwa sasa kutokana na adhabu inayomtaka kutojihusisha na soka mwaka mzima.
“Yeye anaongea lakini hajatuletea tamko lake rasmi na ataongea hukohuko, lakini kwetu tunatambua adhabu iko palepale,” alisema katibu huyo.
Alipoulizwa iwapo Muro ataanza kazi itakuwaje, Mwesigwa alisema: “Siwezi kusemea tuhuma za ‘kama’ lakini ieleweke iwapo ikitokea, nadhani anajua adhabu yake na kwa kuwa halijatokea (kufanya kazi kama alivyotamba) tuliache kwanza.”
Katibu huyo wa zamani wa Yanga, alisema Muro alipewa barua ya hukumu ambayo nakala yake ipo kwa waajiri wake, Klabu ya Yanga ambayo ilitumwa kwa katibu, Baraka Deusdedit.
No comments:
Post a Comment