Saturday, August 6, 2016

WAJUMBE WATATU WAFUTWA UANACHAMA YANGA

Wanachama wa Yanga wamepitisha kwa pamoja kufutwa kwa uanachama kwa wajumbe watatu wa kamati ya utendaji.

Waliofutwa uanachama ni Ayoub Nyenzi, Salum Mkemi na Hashimu Abdallah.

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amewaambia wanachama wa Yanga kwenye mkutano unaoendelea Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, kwamba hana imani nao.

Kutokana na hivyo, zikalazimika kupigwa kura ambazo mwisho ziliamua kufukuzwa kwao.

Abdallah aliyekuwa kwenye mkutano huo aliinuka na kuondoka kwa jazba na kufanya baadhi ya wanachama waliokuwa mkutano hapo kushangaa.

Hivi karibuni, kumekuwa na taarifa ya kutoelewana kati ya uongozi na baadhi ya wajumbe hao wa kamati ya utendaji.

Uongozi ulilalama wajumbe kutaka posho kwenye vikao kama wakikutana lakini wajumbe hao .

No comments:

Post a Comment