Thursday, August 18, 2016

YANGA INA DENI LA BILIONI 5.4

Klabu ya Yanga ipo katika wakati mgumu kifedha baada ya taarifa zao za mapato na matumizi kuonyesha   deni la  Sh 5.4 Bilioni . Taarifa hiyo inaeleza kuwa Yanga imekopa kiasi cha  Shillingi 1.5 Bilioni kwa msimu wa 2015/16 ili kuziba pengo lilijitokeza katika bajeti yao kitendo ambacho kimefanya deni hilo lifikie Sh 5.4 Bilioni.

“Kwa miezi 12 tumekuwa na Sh 1.5 Bilioni ambayo klabu imekopa bila riba, na imekuwa ikikopa kwa miaka kadhaa na imeshindwa kulipa,” ilisomeka taarifa hiyo.

“Mkopo unatoka kwa mwanachama mmoja wa timu ambaye hadi sasa kachangia Sh 1.5 Bilioni na kwa miaka 10 mkopo umefikia Sh 5.4 Bilioni,’’ilieleza taarifa hiyo.

Pia imebainika kuwa kwa mwezi huu (Agosti) Yanga itahitaji Sh 500 Milioni kuendesha shughuli zake mbalimbali, ukiacha Sh 88 milioni zinazotokana na udhamini wa Kampuni ya Quality Group.

Licha ya taarifa hiyo kutomtaja mwanachama anayeidai Yanga, Taarifa za ndani zinaeleza kua ni  Quality Group ndiyo inayotoa mkopo huo kwa udhamini wake na imekuwa ikifanya hivyo miaka 10 sasa.

Kutokana na kutokuwepo kwa mapato ya kueleweka Yanga, deni hilo linatarajiwa kuendelea kukua katika miaka miwili ijayo kwani mpaka sasa hakuna marejesho yoyote aliyoanza kufanyika.

Katika mkutano mkuu wa dharura hivi karibuni, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi Quality Group kabla ya kujitoa aliwataka wanachama wa Yanga kubadili mfumo wa uendeshaji ili wamkodishie timu na nembo aiendeshe kwa faida na kuwapa mgao

No comments:

Post a Comment