Sheila Ally, Dar
STRAIKA wa Simba, Danny Lyaga jana aliondoka kwenda Oman kwa ajili ya kufanya majaribio ya wiki mbili na timu ya Oman Club inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza.
Lyanga amechukuwa uamuzi huo baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha Joseph Omog ambapo tangu ligi ianze hajacheza mechi hata moja na hivyo kumuweka katika wakati mgumu hasa kulinda kipaji chake.
Rais wa Simba, Evans Aveva amethibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo na kwamba endapo atafuzu basi wapo tayari kufanya biashara.
"Tumemruhusu kwenda huko na akifanikiwa na kama wao Oman Club watamuhitaji basi tutawasikiliza ofa yao ya kumnunua nasi tutamuuza pasipo tatizo, maana kila kitu ni mazungumzo," alisema Aveva.
Lyanga hapati nafasi kutokana na ushindani mkubwa toka kwa Laudit Mavugo, Ibrahim Ajibu na Fredrick Blagnon.
No comments:
Post a Comment