Sam Allardyce ameteua kikosi chake ya Timu ya Taifa ya England kwa mara
ya kwanza kabisa kitakachowavaa Slovakia kesho Jumapili, na tayari watu
wengi wameonekana kutofurahishwa.
Meneja huyo ameamua kubaki na wachezaji wengi ambao walionesha
kiwango kibovu katika michuano ya Euro, na hali hiyo imewaacha watu
wengi wakijiuliza kama kweli Allardyce ataonesha utofauti wowote dhidi
ya Hodgson kwenye timu hiyo.
Baadhi ya wachezaji hao ni:
Hart, Walker, Cahill, Stones, Rose, Dier, Henderson, Lallana, Rooney, Sterling, Kane.
Bila shaka John Stones inaonekana kabisa atapata nafasi ya kuanza
katika kikosi cha kwanza baada ya kuwa na kwenye kiwango bora kabisa
msimu uliopita na kufanikiwa kijiunga na Manchester City.
Hata hivyo wengi wanajiuliza juu ya uwepo wa wachezaji kama Henderson
na Kane kutokana na kiwango chao kisichoridhisha kwenye Michuano ya
Euro.
Drinkwater ameachwa tena
Washabiki wengi wanajiuliza inakuaje tena mchezaji kama Danny Drinkwater anaachwa halafu Henderson anachukuliwa.
Ni ukweli ulio wazi kwamba msimu uliopita Drinkwater alicheza kwenye
kiwango cha hali ya juu mno bila kusahau kwenye mechi hizi za awali za
msimu huu licha ya kutokuwepo kwa pacha wake N’Golo Kante ambaye
ametimkia Chelsea.
No comments:
Post a Comment