TAARIFA YA PONGEZI.
Mnamo tarehe 06.10.2016 majira ya asubuhi,klabu ya Simba kwa kupitia Msemaji wake Ndg Haji Manara ilitangaza Kamati mpya ya Mashindano.Kamati ambayo itakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha Simba SC inapata mafanikio na kutwaa mataji ya Ligi Kuu Tanzania Bara,Kombe la FA,pamoja na mashindano yote ambayo timu yetu itashiriki.
Katika majina yaliyotajwa,sisi wana SIMBA PLATINUM SUPPORTERS tulisikia jina la mmoja wa wadau wetu ambaye ni Makamo Mwenyekiti wa Tawi hili la SPS na daktari mstaafu wa klabu yetu ya Simba Daktari Cosmas Kapinga
Kutajwa kwa Dk Cosmas Kapinga kama mmoja wa wajumbe wa Kamati Mpya ya Mashindano ni FARAJA kubwa kwa Tawi la SpS na hii inatokana na sisi kuamini uwezo wake ktk masuala mazima ya mchezo wa mpira wa miguu.
Tunamuhakikishia Dokta Cosmas Kapinga kuwa TUTAKUWA NAYE BEGA KWA BEGA kwa kila jambo lolote lenye kuonesha umuhimu kwa maslahi ya Simba SC na wana Simba kwa ujumla.
SPS kama Tawi la Simba,inajivunia kuwa na mpambanaji makini na mwenye rekodi safi ndani ya klabu yetu.Tunasema hivyo kwa kuwa tunamfahamu vema Dokta Kapinga.
Pamoja na hayo,tunawapongeza wote waliochaguliwa kama wajumbe wa Kamati hiyo ya Mashindano na Uongozi wa Simba kwa ujumla.
Tunahitaji mataji mbalimbali ndani ya Simba kwa sasa.
Kila la heri kwa Simba SC
Mungu tubariki wana Simba SC.
IMETOLEWA NA TINGA NAMBA MOJA LA MICHEZO -SPS.
No comments:
Post a Comment