Simba wamepania kufanya mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji, leo wamesikika wakifanya mabadiliko ya kauli mbiu yao ya 'Simba Nguvu Moja' na kuwa 'Simba Mabadiliko'.
Hayo yametokea asubuhi hii kwenye mkutano mkuu baada ya Rais wa klabu hiyo Evance Aveva kusimama ili kufungua mkutano huo ndipo aliposema 'Simba' akitarajia kujibiwa 'Nguvu Moja' katika hali ya kushangaza wanachama hao walijibu kwa pamoja 'Mabadiliko'.
Kabla ya hapo wanachama hao walilipuka kwa furaha pale iliposomwa ajenda ya tisa inayozungumzia maboresho ya mfumo wa uendeshaji huku ikionyesha wazi wanahitaji mabadiliko ya kuondoka kwenye mfumo wa Uanachama na kwenda kwenye Hisa.
Tayari mfanyabiashara Mohamed Dewji 'Mo' ameshaweka wazi nia yake ya kutaka kuwekeza katika klabu hiyo kwa kutoa kiasi Sh 20 Bilioni.

No comments:
Post a Comment