Sunday, July 24, 2016

PLUIJIM AJAKATA TAMAA KWA MEDEAMA

Tausi Salum

KOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga, Hans van der Pluijm, amesema katika maisha ya soka ajakata tamaa, hivyo katika mchezo wao ujao dhidi ya Medeama lolote linaweza kutokea.

Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Pluijm alisema kuwa wako vizuri kwa ajili ya chochote kilichotokea, inawezekana ikatokea kilichotokea hapa nchini au kukawa na mabadiliko kwa klabu yake kupata ushindi.

Pluijm alisema katika mpira lolote linaweza kupatikana kwa kuwa wamejipanga kuvanya vizuri kikosi chake kina hali kubwa ya ushindi, hivyo kupata kwake ushindi katika mchezo huo ujao ni muhimu na wanautarajia kwa sababu wamejipanga vizuri.

"Katika maisha ya soka uwa sikati tamaa  nina amini kila jambo linaweza kutokea, matokeo kama yaliyotokea haoa nchini au tukashinda, maana hata kupata matokeo ya 1-1 kama ya hapa kwetu ugenini ni nafasi nzuri, lakini kushinda nako ni muhimu zaidi"alisema Pluijm.

Kikosi cha Yanga kimeondoka majira ya saa 10, usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Medeama.

Yanga imeondoka ikiwa chini ya Mkuu wa Msafara Hussein Nyika ambaye ni pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo.

Mchezo kati ya Medeama dhidi ya Yanga utachezwa kwenye uwanja wa Essipong Sports uliopo kwenye mji wa Sekondi, Ghana. Mechi hiyo itakuwa chini ya mwamuzi wa kati Redouane Jiyed atakayesaidiwa na Mohamed Lahmidi na Hicham Ait Abboou.

Yanga itaingia uwanjani kupambana na Medeama ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare kwenye mchezo wa awali ilitoka sare ya kufungana goli 1-1 na kujiweka kwenye mazingira ya kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Klabu hiyo ya mtaa wa Twiga na Jangwani, ipo nafasi ya mwisho kwenye Kundi A ikiwa na pointi moja.

No comments:

Post a Comment