Monday, July 25, 2016

Simba ni kombinesheni na mbinu kwa kwenda mbele

                                      

KOCHA Mkuu wa Joseph Omog akiendelea na programu ya kutengeneza kombinesheni, amepanga kuanza na programu ya mazoezi ya kimbinu kwa wachezaji wake ikiwa ni kuimarisha zaidi timu hiyo.

 

Simba wameweka kambi mjini Morogoro  ikiendelea na Program kwa ajili ya maandalizi ya msimu  ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaoanza Agosti 20.

 

Omog  amekuwa makini na program yake huku akihakikisha anatengeneza kombinesheni kwa wachezaji wake wapya ili kuendana na waliowakutana katika kikosi hicho.

 

Mcameroon huyo anaendelea na programu hizo huku akiwa na baadhi ya nyota wapya waliowasajili kwa ajili ya msimu ujao  ni Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim, Mzamiru Yassin na Hamad Juma.

 

Licha ya hayo pia kuna wachezaji wanne wako katika mchujo ambao ni Wakongo, Janvier Bokungu, Moussa Ndusha, Muivory coast, Blagnon Fredric na Mzimbabwe, Method Mwanjali.

 

Kocha huyo alisema  hivi sasa amezielekeza nguvu zake huko kwa kuhakikisha wachezaji wake wanashika mbinu mbalimbali anazowapa,

anataka kuona timu inacheza soka la pasi za haraka wakati timu ikiwa ina mpira ikishambulia kwenye goli la wapinzani.

 

Alisema yuko makini wakati timu inapopoteza mpira, lakini kwa pamoja wote wanatakiwa kukaba kwa kuanzia washambuliaji, viungo na mabeki.

 

“Baada ya kufanya kazi yangu ya awali ikiwemo Program ya kuwaweka wachezaji wangu kuwa fiti, ninahakikisha kutengeneza kombinesheni kwa wachezaji wake kabla ya Ligi,” alisema .

 

Alisema anahitaji kuona wachezaji wake wanacheza soka la pasi za haraka , kwa kushambulia kwa timu mpinzani pamoja na kukaba pia wasipoteze mpira.

 

 

No comments:

Post a Comment