Monday, July 25, 2016

YANGA IMEENDELEA NA MAZOEZI

YANGA imeendelea na mazoezi Leo usiku  imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa shule ya Bohar mjini hapa kujiandaa na mchezo wa  Kesho dhidi ya wenyeji, Medeama ya Ghana.

Timu iliyowasili Ghana tayari kwa mchezo hao huo ambao utapigwa katika  Kesho , timu hiyo imepania kushinda mechi hiyo kufufua matumaini ya kwenda Nusu Fainali.

Yanga iliyondoka bila ya wachezaji wao watatu wakiwemo beki Mtogo  Vincent Bossou abaye ameeachwa Dar es Salaam,  anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano, wengine wakiwa ni viungo Geoffrey Mwashiuya na Deus Kaseke ambao ni majeruhi.

Kocha Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans van der Pluijm amesema pengo la Bossou litazibwa na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye yuko fiti na kuicheza mchezo huo.

Amesema amefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika michezo iliyopita ambapo kazi yake amemaliza jijini Dar es Salaam, kazi iliyobakia ni vijana wake kufanya kazi.

“Kuna viungo wa kutosha, sifurahii kuwakosa Kaseke na Mwashiuya, lakini kwa kuwa hawapo kwa sababau ambazo zipo nje ya uwezo wetu, wengine watacheza badala yao,”amesema .

Kocha huyo amesema baada ya kumaliza kazi yake, hivyo anachokifanya ni kutoa maelekezo kwa wachezaji wake na kuhitaji vijana wake kushambulia na kuzuia.

Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na MO Bejaia pointi tano, Medeama pointi mbili, wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia.

 

 

No comments:

Post a Comment