Sunday, August 21, 2016

BLAGNON ATUMA SAALAM LIGI KUU TANZANIA BARA,,AMUAMBIA TAMBWE AJIANDAE

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba Fredrick Blagnon ametuma salaam kwa washambuliaji wa ligi kuu Tanzania bara jana baada ya kuifungia timu yake goli muhimu.
Katika mchezo huo muhimu ambao ulihudhuriwa na maelfu ya mashabiki wa Simba SC, Blagnon alifunga akitokea benchi kuchukua nafasi ya kiungo mshambuliaji wa Simba aliyesajiliwa kutoka Mwadui FC.
'Nimekuja kufanya kazi Tanzania,nafikiri ni wakati muafaka wa kurejesha furaha ya mashabiki wa Simba SC ambayo imepotea kwa takriban misimu minne,,nimeanza kwa kufunga na mungu akipenda nitaendelea kufunga' alimaliza mshambuliaji huyo akiongea na blog hii.

Wakati huo huo kikosi hicho cha mabingwa wa zamani wa ligi kuu Tanzania bara kimesema kuwa Ibrahim Ajib hakuwa na tatizo lolote kwani baada ya kupewa kadi nyekundu mechi za msimu uliopita alikosa mechi ya Majimaji, Mtibwa Sugar ,pamoja na Jkt RUvu.

No comments:

Post a Comment