Saturday, August 27, 2016

BIN KLEB AREJESHWA YANGA

Na Tausi Salum
MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Manji, amemrehesha aliyewahi kuwa mwenyekiti wa kamati ya mashindano Abdallah Bin Kleb, kuwa mjumbe katika kamati hiyo mpya.
Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Baraka Deusdedit, alisema kuwa Manji ameunda Kamati mpya ya mashindano baada ya kujizulu ya aliyekuwa mwenyeji wa kamati hiyo Isaac Chanji, kujiuzulu.
Deusdedit, alisema kwa mamlaka aliyonayo Manji kama mwenyekiti amemteuwa  Mwenyekiti mpya ambaye ni  Mhandisi Paul Malume, ambaye pia anaingia kwenye Kamati ya Utendaji kama Mjumbe Mteule.
Wajumbe wa Kamati hiyo ni Abdallah Bin Kleb, Mustafa Ulungo, Mhandisi Mahende Mugaya, Jackson Mahagi, Samuel Lukumay na Hussein Nyika.
Wengine ni Athumani Kihamia wa Arusha, Felix Felician Minja wa Mwanza, Leonard Chinganga Bugomola wa Geita, Omar Chuma, Hussein Ndama, Hamad Ali Islam wa Morogoro, Yusuphedi Mhandeni, Beda Tindwa, Moses Katabaro na Roger Lemlembe

No comments:

Post a Comment