Sunday, August 7, 2016

SIMBA KUMENYANA NA AFC LEOPARDS KESHO

Na Tausi Salum

Klabu ya Simba inayo furaha kubwa sana kuwaarifu imeshakamilisha maandalizi yote ya mechi ya kesho dhidi ya timu ya AFC Leopards ya nchini Kenya.

Mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es salaam

Mkuu wa Idara ya Habari wa klabu ya Simba Haji Manara, alisema kuwa mehi hiyo ya kimataifa itatanguliwa na burudani mbali mbali za muziki zitakazoongozwa na bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta pamoja na wasanii wa muziki wa kizazi kipya.

Mbali ya burudani hizo.pia kutakuwa na shamra shamra nyingine.zitakazonegesha kilele cha wiki ya sherehe zetu.zinazojulikana kwa umaarufu wa Simba Day.

Klabu pia itatumia mechi ya kesho kuwatambulisha wachezaji wote watakaotumika kwenye msimu ujao wa ligi 2016|17.wakiwemo wale wapya waliosajiliwa msimu huu.

Sanjari na hayo kesho tutazindua rasmi jezi mpya za msimu na pia zitaanza kuuzwa pale uwanjani Taifa kwa thamani ya shilingi elfu ishirini kwa jezi moja.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ataongoza viongozi mbali mbali wa kitaifa kwenye sherehe hizo muhimu ambazo pia ni maadhimisho ya miaka themanini toka kuanzishwa kwa klabu yetu.

Kiingilio kwenye mechi hiyo ni shilingi 5000 kwa mzunguko.10000 kwa viti vya orange.15000 kwa VIP C.20000 kwa viti vya VIP B na shilingi 25000 kwa VIP A.

Tunawaomba sana watu watakaokuja uwanjani kesho wajihadhari na matukio yote yatakayoashiria uvunjifu wa amani.ili kutoa fursa kwa watu kupata burudani na kuona kwa raha mchezo huu muhimu ambao ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom na kombe la Shirikisho.

No comments:

Post a Comment