- 1. SALA ZA UFUNGUZI
- 1.1. Sala ya Wakristo ilisomwa.
- 1.2. Sala ya Waislam ilisomwa.
- 2. UFUNGUZI WA MKUTANO ULIFANYWA NAMWENYEKITI, WA young africans sports club SAA 5 ASubuhi.
- 3. kupitishwa kwa ajenda kulitolewa na Mwenyekiti, WA YOUNG africans sports club SAA 5:30 ASUBUHI.
- 3.1. Wanachama walikubaliana kuipitisha Ajenda.
- 4. MASUALA YA SOKA – yalisomwa na Mwenyekiti, wa young africans sports club.
- 4.1. Msimu uliopita, Klabu:
- 4.1.1. Ilipata ushindi wa Ngao ya Jamii;
- 4.1.2. Ilikuwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2015 /2016 Vodacom;
- 4.1.3. Ilikuwa mshindi wa Kwanza wa Kombe la FA;
- 4.1.4. Ilifikia raundi ya tatu ya Ligi ya Mabingwa na ikapoteza mchezo wa marudiano nchini Misri; na
- 4.1.5. Ilifikia hatua ya Kombe la Shirikisho na Hatua ya Makundi baada ya karibu miaka 20 kupita bila kufikia hatua hiyo ya makundi ya Mashindano ya Kimataifa ya Bara la Afrika.
- 4.1.6. Wakati Klabu ya Young Africans Sports ni klabu pekee ambayo inaiwakilisha Jamhuri ya Tanzania katika mashindano ya Kimataifa, yaani katika Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup Group Stage), kuna changamoto kubwa mbele kwa Klabu katika kufikia hatua ya mbele zaidi katika maendeleo ya soka na inategemewa kuchukua miaka isiyopungua minne ili kufika katika hatua za nusu fainali za Mashindano ya Bara la Afrika na miaka ipatayo sita ya juhudi za kuweza kufika katika fainali za mashindano hayo.
- 4.2. Mwenyekiti, aliwafahamisha Wanachama kwamba pamoja na kushindwa katika mashindano hayo ya Afrika mwaka huu, lakini imani kubwa ya Wanachama na vitega uchumi vyao katika Yanga vinaonyesha kwamba hatimaye baada ya miaka kumi Klabu inaonyesha mwelekeo mzuri.
- 4.3. Mwenyekiti, kwa niaba ya Klabu, alielezea kufurahishwa na hatua za serikali, wakati wa mchezo dhidi ya TP Mazembe, kwa kuhakikisha kunakuwa na mazingira ya amani katika Uwanja wa Taifa, kwa kuondoa gharama za malipo ya uwanja na kwa kuzuia njama za Shirikisho la Soka nchini (TFF) kutaka kuweka kuifanya Klabu ilipe kodi ambazo hazikuwa na msingi.
- 4.4. Mwenyekiti, aliendelea kwamba serikali iliunga mkono kwa kuruhusu Klabu kuwa na mchezaji wa 12, yaani wapenzi wa soka walioingia bure kuitazama mechi dhidi ya TP Mazembe ambapo walijitokeza kwa wingi licha ya kwamba Yanga haikushinda mchezo huo. Kitendo hicho kiliifanya Klabu kuonyesha umoja na uzalendo wa Tanzania, jambo ambalo lilikuwa muhimu katika kuipa moyo timu.
- 4.5. Mwenyekiti, aliongeza kusema kwamba katika mechi iliyofuatia dhidi ya Medeama SC kutoka Ghana, baada ya Rais wa TFF kusema kwamba shirikisho lake lingesimamia michezo yote ya Kimataifa ya timu za soka za Tanzania, Klabu ililazimika kuwatoza kiingilio mashabiki japokuwa kilikuwa cha chini. Hata hivyo, Yanga ilitoa ombi kwamba fedha zilizopatikana kutokana na kiingilio, zitunzwe na uongozi wa Uwanja wa Taifa chini ya Wizara ya Michezo na kuilipa Yanga fungu lake kwa cheki.
Ombi la Yanga lilikubaliwa na Wizara ya Michezo na licha ya makusanyo ya Sh. Milioni 118.2 kutoka kwenye viingilio, kitu cha kushangaza ni kwamba Klabu ilipata Sh. Milioni 59.2 tu (pamoja na kuondolewa kwa VAT) na licha ya kuomba kuweko mashine za kieletroniki za kutolea risiti (EFD) kutoka Wizara ya Michezo, TFF, na magari ya wagonjwa kutoka Muhimbili ili Klabu iweze kudai sehemu ya kodi, vitu hivyo havikutolewa na Yanga haiwezi kurudisha gharama za VAT zilizotokana na kodi ambazo zingekuwa Sh. Milioni 10.71 za ziada kwa Klabu.
- 4.6. Mwenyekiti, pia alionyesha kushangazwa kwake kwa nini TFF haionyesha msimamo wa kuunga mkono mafanikio ya Klabu kama ambavyo mashirikisho ya nchi nyingine yanavyofanya. Akielezea hilo, alitoa mfano kwamba;
- 4.6.1. Rais wa TFF katika mkutano wake na Waandishi wa habari alisema kwamba mchezo wa TP Mazembe, shirikisho lingekuwa na wajibu wa kusimamia matayarisho ya mechi zote za Kimataifa za Yanga. (Kiambatisho cha 1 cha Taarifa ya Rais wa TFF iliyotolewa na kupitishwa);
- 4.6.2. Mwenyekiti, wa Young Africans alikubali kuingia kwa shirikisho hilo kwa niaba ya Klabu, kwamba TFF ibebe gharama za matayarisho yote wakati wa kuikaribisha Medeama SC, na gharama zilizotokana na safari ya Yanga kwenda Ghana – jumla ya Sh. Milioni 170, bado hazijalipewa na TFF. Yanga ilibidi kulipa fedha hiyo kwani ingejikuta ikifungiwa na CAF. (Kiambatisho cha 2 cha Taarifa ya Yusuf Manji na Gharama zote Husika iliyotolewa na kupitishwa);
- 4.6.3. Mwenyekiti, aliwaeleza Wanachama kwamba baada ya kuchaguliwa kwake mara ya kwanza mwaka 2013 Yanga ilijiandikisha katika VAT tangu mwaka huo, hata hivyo, hadi sasa TFF haijailipa Klabu kuhusu tiketi za VAT, kukodisha uwanja, na kadhalika, lakini imekuwa ikiitumia VAT kwa kujinufaisha kama vile kukodisha nyumba, na kadhalika (kuhusu kodi). Iwapo TFF ingefuata tu sheria za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na kukusanya mapato kutokana na fedha inayoingia na kutoka kwa msingi wa VAT, Klabu ingekuwa na Sh. Milioni 382 ambazo TFF inadai inazilipa TRA bila ya kuwepo ushahidi wa Klabu kuzidai fedha hizo kutoka TRA (Kiambatisho cha 3 cha VAT kutoka TFF kilichotolewa na kupitishwa);
- 4.6.4. Mwenyekiti, aliwakumbusha Wanachama kwamba Katiba ya Yanga, na marekebisho yake kwa mujibu wa Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika mnamo 2013 na 2014 vililenga kuleta mabadiliko katika Katiba hiyo ikiwemo Kamati ya Utendaji iteuliwe na Mwenyekiti, na MakamuMwenyekiti, ili kupunguza msuguano katika Klabu kama ilivyokuwa hapo nyuma kabla ya kuingia kwake katika Klabu, kati ya Mwenyekiti, na Makamu Mwenyekiti,, jambo ambalo lilisababisha Klabu kufungwa na Simba magoli 5 kwa 0, lakini mwaka huu magoli manne yakiwa tayari yamelipwa na Klabu dhidi ya Simba. Hata hivyo, TFF iliandika ikipinga maamuzi ya Wanachama ikitoa sababu za kuchekesha za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) wakati kuna Klabu zinazomilikiiwa na watu binafsi au taasisi mbalimbali ambazo hazina tatizo lolote, wakati ambapo Vilabu vya Wanachama viko tayari kumilikiwa kibinafsi.(Kiambatisho cha 4 cha barua TFF inayokataa kuafiki umauzi wa wanachama iliyotolewa na kupitishwa);
- 4.6.5. Mwenyekiti, aliwasomea wanachama marekebisho yaliyokubaliwa ya Katiba ambayo yalikubaliwa wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wanachama wa Yanga wa mwaka 2013, kwamba “… baada ya uchaguzi wa Mwenyekiti, na Makamu Mwenyekiti, kwa pamoja watateua Kamati ya Utendaji ambayo watakuwa na uwezo wa kuindoa au kuteua nyingine mpya” lakini ilikataliwa na TFF; na
- 4.6.6. Mwenyekiti, aliwasomea wanachama marekebisho yaliyokubaliwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Yanga wa Juni 1, 2014 ambapo ulikubali kuanzishwa kwa Kamati ya Nidhamu kama ilivyotakiwa na TFF kutokana na maelekezo kutoka FIFA ili Yanga iweze kushiriki katika Ligi Kuu lakini ikakataliwa na TFF. Hili halikuifanya Yanga ionekane kupingana na Sheria za Fifa tu, lakini ikiwa haina chombo cha kushughulikia masuala la Klabu hiyo kuhusiana na nidhamu;
- 4.6.7. Mwenyekiti, aliendelea kwamba mabadiliko yaliyofanywa na wanachama kwenye Katiba yao yalipelekwa hata kwa Msajili wa Michezo ambapo hadi leo ni miaka mitatu hadi minne imepita bila Klabu kujulishwa chochote, jambo ambalo linamshangaza Mwenyekiti, iwapo serikali inaweza kuruhusu taasisi kama vile za kisiasa au wadhamini kuendesha shughuli zao bila Msajili wa Michezo kutambua Klabu husika, ambapo Klabu haijawasilisha mahesabu yake kwa serikali kwa miaka minne sasa.
- 4.6.8. Mwenyekiti, aliripoti kwa Wanachama kwamba Uchaguzi Mkuu wa Yanga unahitajika kuendeshwa na kusimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga hata kwa mujibu wa Katiba ya 2010 ambapo Yanga ilikuwa na bajeti yake kulingana na sera za Klabu. Yanga imedhamiria kuhakikisha shughuli zake zina faida kwa wanachama wake na si mtu mwingine na ndiyo maana hatukukubali Uchaguzi Mkuu kufanywa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kama ilivyotaka kwamba Yanga ililazimika kwanza kulipa Sh. Milioni 9 kwa ajili ya posho, tiketi za ndege na gharama za hoteli kwa maofisa wa TFF kutoka Kagera kuja Dar es Salaam. Hii ni bila kujumuisha gharama halisi za uchaguzi. Hata hivyo, Yanga iliendesha uchaguzi wake kwa gharama zake, uchaguzi uliokuwa huru na wa haki (chini ya Katiba ya 2010) kwa kutumia Sh. Milioni 10 katika muda wa siku 14. (Kiambatisho cha 5 cha barua ya maelekezo ya TFF, barua ya TFF kuhusu posho na taarifa ya gharama za Yanga ambayo ilitolewa na kupitishwa);
- 4.6.9. Hitimisho la Mwenyekiti, ni kwamba viongozi walioshindwa wa Yanga ambao sasa wanaiendesha TFF, wanataka kuiendesha Yanga au kuihujumu. (Kiambatisho cha 6 cha Celestine Mwesiga akiishitaki Yanga, iliyotolewa na kupitishwa);
- 4.6.10. Mwenyekiti, aliomba mwongozo kutoka kwa Wanachama katika kuendesha shughuli za Klabu kwani pamoja na Jerry Murro kupeleka ripoti ya njama za TFF na Msajili wa Michezo katika uchaguzi wa Yanga, hakuna mtu yoyote katika Klabu aliyehojiwa wala hakuna afisa yeyote wa TFF au Wizara ya Michezo aliyesimamishwa, hali inayoonyesha utendaji kazi wa serikali ya sasa.
Mwenyekiti, aliendelea kusema kwamba Klabu imefahamu kupitia vyombo vya habari kwamba Jerry Murro amesimamishwa katika shughuli za soka kwa mwaka mmoja, pamoja na kwamba msingi wa hukumu hiyo haujaletwa kwa Klabu kimaandishi. Hivyo, Mwenyekiti, alishangaa kutokuwepo kwa fursa ya kujielezea katika soka la Tanzania.
Mwenyekiti, alisema kwamba kuna wakati anasema kwa niaba ya Klabu na kuna wakati anakuwa anasema mambo yake kama mtu binafsi. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jerry ana haki ya kujieleza kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anapozungumza kwa niaba ya Yanga kama Mwenyekiti, yeye ndiye msemaji mkuu na kiongozi mkuu.
Mwenyekiti, alitoa fursa kwa Wanachama kutoa maoni yao.
Hakuna Mwanachama aliyetoa maoni yoyote.
- 4.6.11. Mwenyekiti, aliwajulisha Wanachama kwamba kwa mara nyingine TFF ilikuwa imesaini bila ya idhini ya Yanga mkataba mpya wa kituo cha Televisheni cha Azam kurusha Matangazo ya Ligi Kuu ya Vodacom, jambo alilosema litapunguza idadi ya watu kuingia viwanjani. Mwenyekiti, alisema kwamba ni kweli Ligi Kuu katika muundo wa sasa inamilikiwa na TFF, lakini Wachezaji na nembo ni mali ya Yanga na kwamba kuzitumia vitu hivyo kwa ajili ya kuingiza fedha ni jambo haramu na kwamba ufumbuzi utapatikana mahakamani ambapo TFF na Azam TV watabidi kujibu na kufidia hasara inayotokana na kupoteza mapato ya Klabu.
Wanachama walikubaliana juu ya hilo kwa kauli moja.
- 4.6.12. Mwenyekiti, alitoa ombi kwamba kama kuna uwezekano, akiwa Mwenyekiti, wa Yanga, bidhaa za Azam zisusiwe hadi mgogoro huo wa kisheria umalizike.
Wanachama walikubaliana na hoja hiyo kwa kauli moja.
- 5. MAPATO NA MATUMIZI YA YANGA kama yalivyotolewa na Mwenyekiti, wa young africans sports club.
- 5.1. Mwenyekiti, alieleza kwamba kila mwaka mapato ya Yanga hutokana hususani na wadhamini, viingilio, michango na mikopo. Mapato kamili kwa miezi 12 kutoka kampuni ya TBL yalikuwa Tshs 500ml, VodaCOM (wadhamini wa Ligi Kuu) Tshs 73ml, biashara ya kuuza na kununua wachezaji Tshs 74ml. Mapato ya viingilio mwaka jana yalikuwa Tshs 678 ml- hivyo mapato kwa jumla mwaka jana yalikuwa Tshs 1.325 B.(Kiambatisho cha 7 cha taarifa ya mapato iliyotolewa na kupitishwa);
- 5.2. Mwenyekiti, aliendelea kuwajulisha Wanachama kwamba gharama za matumizi kwa jumla kwa miezi 12 iliyopita (ambayo ni pamoja na mishahara, kununua Wachezaji, bonasi, usafiri, na kadhalika) yalikuwa Tshs 2.879 B. (Kiambatisho cha 8 cha taarifa za matumizi iliyotolewa na kupitishwa);
Mwenyekiti, alisema kwamba mnamo miezi 12 iliyopita kumekuwepo na pengo la Tshs 1.5 bililoni lililo sababishwa na Klabu kukopa bila kukatwa riba. Na mnamo miaka 10 iliyopita imekopa na kushindwa kulipa Tshs 11.676 B. (Kiambatisho cha 9 na 10 cha taarifa ya mkopo iliyotolewa na kupitishwa);
Mwenyekiti, alifafanua kwamba mkopo uliotajwa hapo juu ni kutoka kwa Mwanachama mmoja alioutoa kwa Klabu ambao ni Tshs 1.490 B na katika kipindi cha miaka 10 ni 11.676 B (Kiambatisho cha 10 na miaka 10 ya Taarifa ya Mchango waMwenyekiti,).
Mwenyekiti, aliripoti kwamba mwezi Agosti, Klabu inahitaji kiasi cha Tshs 500 million licha ya Quality Group kudhamini kupitia kampuni yake Tshs 88 million bila kuwepo na michango yoyote. (Kiambatisho cha 11 kilichotolewa na kupitishwa).
Mwenyekiti, alitahadharisha kwamba iwapo Klabu inapata hasara kila mwaka, dhana ya kuanzishwa kwa kampuni ambapo Wanachama wangekuwa na hisa ina maana Wanachama wangeikopesha Klabu mwaka jana kiasi cha Tsh 1.5 B na mwaka huu, kutokana na kupanda kwa matumizi, kiasi hicho kingekuwa Tshs 1.98 B- bila kufanya hivyo itajikuta ikiuza mali zake ambazo zina umuhimu wa kihistoria kwa Klabu yenyewe na kwa Taifa na kwa Kaunda kwa kufahamu kwamba mambo hayo yalianzishwa na Mzee Karume, Mwalimu Nyerere na kadhalika.
- 6. SHUKURANI KWA WAJUMBE WENYE KUONDOKA WA KAMATI YA UTENDAJI, MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU NA KUWAKARIBISHA WAJUMBE WAPYA WA KAMATI YA UTENDAJI KAMA ILIVYOTOLEWA NA MWENYEKITI, WA young africans sports club
- 6.1. Mwenyekiti, alielezea furaha yake kwa wajumbe wanaomaliza muda wao wa Kamati ya Utendaji ambao alifanya nao kazi hadi sasa ambapo Yanga inashiriki katika hatua za makundi za Kombe la Shirikisho baada ya miaka 18 ambapo hawakuomba posho hata siku moja. Hao ni:
- • Isaac Chanji Mhandisi
- • Arms Rajabu Katibu Mkuu wa zamani
- • David Seki Mkurugenzi wa Kikundi cha Original Comedy.
- • G. Fumbuka Bora Uziyaji wa Hisa kwneye DSE
- • Waziri Barnabas Bwana Fedha Mkuu wa NMB
- • Sam Mapande Wakili wa Mahakama Kuu
- • Mohamed Nyengi Meneja wa Taifa wa Tawi wa Stanbic
- • Moses Katabaro Mfanyabiashara.
Mwenyekiti, alisema kwamba hawa walikuwa ni chaguo lake: i)kuanzisha kampuni (jambo ambalo haliwezekani kwa vile Klabu ilikuwa inajiendesha kihasara); ii) kujenga uwanja (haiwezekani kwa vile ombi la kupanua eneo la uwanja wa Kaunda kulikataliwa na mamlaka husika);iii) kuimarisha uongozi na nidhamu, mambo yaliyofanikiwa lakini Klabu bado ilijiendesha kihasara; na iii) kutayarisha kizazi cha vijana kurithi shughuli za Klabu (lakini bado mambo hayajawa tayari kwani Klabu inahitaji viongozi hawa kutayarishwa na Wanachama wa kuwahamasisha badala yake wanaelekeza nadhari yao kwake badala ya kufahamu kwamba Yanga ni watu na si mtu mmoja, jambo ambalo linamkera).
- 6.2. Matokeo ya washindi wa uchaguzi ya 12 Juni, 2016 yalitangazwa kupitia Ripoti ya Mwenyhekiti wa Kamati za Uchaguzi (Kiambatisho cha 12 ilichotolewa na kupitishwa).
- • Yusuf Manji Mwenyekiti, (kura 1468)
- • Clement M/Mwenyekiti, (kura 1428)
- • Siza Lyimo Mjumbe K/Utendaji (kura 1027)
- • Ayoub Nyenzi Mjumbe K/Utendaji (kura889)
- • Hashim Abdallah Mjumbe K/Utendaji (kur 727)
- • Tobias Lingalangala Mjumbe K/Utendaji (kura 889)
- • Salum Mkemi Mjumbe K/Utendaji (kura 894)
- • Omar Said Mjumbe K/Utendaji (kura 1069)
- • Samuel Lukumayi Mjumbe K/Utendaji (kura 818)
- • Hussein Nyika Mjumbe K/Utendaji (kura 770)
- 6.3. Mwenyekiti, aliwakaribisha rasmi na kuwajulisha Wanachama wapya wa Kamati ya Utendaji kwamba mkutano wa kwanza wa Kamati hiyo uliokuwa chini ya MakamuMwenyekiti,, kuanzisha barua pepe na kuwaomba wa kutoa historia zao fupi muhimu kikazi (CVs) ili kuendana na majukumu kama ya Kamati ya Utendaji iliyopita (Kiambatisho cha 13 dondoo za mkutano kama zilivyotolewa na kupitishwa).
- 6.4. Mwenyekiti, alielezea masikitiko yake kwamba ni CV tatu tu zilipokelewa kutoka kwa wajumbe wapya wa Kamati ya Utendaji na kuna kati yao aliyetoa barua pepe yake, hivyo bado hajui uwezo wao na hivyo kumfanya yeye na MakamuMwenyekiti, kuonekana ni watu wawili tu wanafanya kazi katika Klabu, jambo ambalo si jema.
- 6.5. Mwenyekiti, alimwomba Kaimu Katibu Mkuu kutoa maelezo yake kuhusu maofisa waliochaguliwa. (Kiambatisho cha 13 cha dondoo za mkutano kama kilivyosambazwa, kutolewa na kupitishwa).
- 6.6. Katibu Mkuu alitoa ripoti kwamba:
Katibu Mkuu, kwa ripoti ya Katiba ya Yanga ilisema wasemaji wakuu wa Klabu ya Yanga ni Mwenyekiti,, Katibu Mkuu na Afisa Habari. Kumekuwepo na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye kwa wakati tofauti amezungumzia masuala ya Wachezaji kwenye vyombo vya habari. Ndugu Salum Mkemi, aliongea na kituo kimoja cha Radio (EFM) tarehe 04 Agosti 2016 na kushutumu uongozi wa Mwenyekiti, wetu kwamba hauwatendei haki na kuwanyanyasa na kutowaheshimu Wanachama. Kumekuwepo na shutuma kwamba kuna baadhi ya Wajumbe wamekuwa wakichochea migogoro ndani ya timu yetu.
Katibu Mkuu, aliendeleza kueleza mchezo wa Kombe la Shirikisho la Afrika (CAF Confederation Cup) kati ya Yanga na Medeama SC kutoka Ghana, uliochezwa hapa jijini Dar es Salaam, baada ya mchezo huo kumalizika zoezi la uhakiki wa mauzo ya tiketi ulianza mara moja. Kwa nia njema na ya dhati ya kutaka usimamizi mzuri wa fedha za mapato pamoja na kuisadia Serikali kukusanya mapato yake vizuri katika mchezo huo, Klabu iliomba fedha hizo zibaki polisi kwa usalama zaidi, malipo yafanyike siku hiyo hiyo kwa mfumo wa hundi lakini ilitokea sintofahamu ambapo baadhi ya Wajumbe ya Kamati ya Utendaji ya Yanga walinivamia kwa kikundi huku wakinishinikiza mgawanyo wa mapato hayo ufanyike uwanjani na hivyo kukosa usimamizi sahihi wa fedha. Jambo hili lilileta tafrani na mkanganyiko mkubwa. Ikumbukwe tu kwamba nia madhubuti ya uongozi ni kulinda maslahi mazima ya Yanga. Wajumbe hao ni pamoja na Hashim Abdallah, Salum Mkemi na Ayoub Nyenzi.
Katibu Mkuu, ka ripoti akipenda kutoa taarifa nyingine kuwa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Africa (CAF Confederation Cup) kati ya Yanga na TP Mazembe jijini Dar es Salaam tulifanikisha azma yetu ya kuweza kupata mchezaji wa 12 nikimaanisha mashabiki wengi wa kushangilia timu yetu. Alishukuru mamlaka za kiserikali husika, hususani jeshi la Polisi kwa kuimarisha amani katika mchezo huo. Bado nasisitizia posho za askari hao waliotumika ambapo Ndugu Hashim Abdallah (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji) akiwa kiongozi wao kufuatilia posho hiyo kiasi cha Tshs 5,000,000. Posho ambayo haikuwa kihalali kwani tulikuwa tumeshapata ushirikiano kutoka Serikalini wa kutusaidia zoezi zima la usalama.
- 6.7. Katibu Mkuu, ka ripoti kwamba kwa mujibu wa Katiba ya 2010, hana mamlaka ya kushughulika na masuala haya na aliwataka waliokuwepo kujitetea na wanachamawana haki ya kuwavua uanachama wahusika na kwamba nafasi zao zilizo waziMwenyekiti, anaweza kuzijaza kwa kuwateua watu wengine.
- 6.8. Siza Lyimo – alijitete na Wanachama walipiga kura ya kumpa onyo na ajirekebishe; Ayoub Nyenzi hakuwepo kwenye mkutano na Wanachama walipiga kura kumvua uanachama; Hashim Abdallah aliondoka kwenye mkutano na wanachama walipiga kura kumvua uanachama; Salum Mkemi hakuwepo na wanachama walipiga kura kumvua uanachama. Ilikubalika kwamba nafasi husika zilizobaki wazi zitajazwa kwa kufanyika uchaguzi mdogo wakati muafaka.
- 7. MATUKIO MENGINE
- 7.1. Mwenyekiti, aliwafahamisha Wanachama kwamba tajiri mkubwa zaidi nchini Tanzania, Mohamed Dewji, alikuwa katika mchakato wa kuwekeza kwa ajili ya kuimiliki Klabu ya Simba, ambapo alimtakia kila la heri katika mchakato huo. Akasema pia kwamba mtu anayeshika nafasi ya pili kwa utajiri nchini, Mzee Bhakressa, yeye tayari ana timu ya Azam, na alimtakika kila la heri pia.
- 7.2. Mwenyekiti, aliwaambia Wanachama kwamba Simba na Azam zitakuwa Klabu zenye kuongozwa na maamuzi ya mtu mmoja na hivyo akasema kwamba kwa mujibu wa Katiba ya 2010 ya Yanga, Klabu hiyo haiwezi kushindana na hivyo aliwataka wanachama kutoa michango yao katika hilo. Mwanzo kabisa alijikaribishwa Abbas Shentemba aliyedai kwamba kulikuwa na mwekezaji mwenye Dola Milioni 30 aliyetaka kuwekeza katika Klabu, lakini hakuwemo katika mkutano huo. Kiasi cha Wanachama 20 walipewa fursa ya kutoa mawazo yao na wote walitoa kauli ya kutaka Klabu auziwe Mwenyekiti.
(Kwa vile huu ni uamuzi mkubwa unatakiwa kupigiwa kura sanduku za kupigia kura ziliiingizwa wakati michango ya Wanachama ilikwa inanedelea)
- 7.3. Mwenyekiti, alifupisha mchango na alisema dhamira yake haitamruhusu kuinunua Klabu. Thamani ya Yanga ni zaidi ya fedha. Ndiyo iliyoanzisha Tanganyika na baadaye Tanzania, kwani waasisi wa taifa hili walikuwa ndani ya Yanga ambapo waliikomboa si Tanzania tu bali Afrika. Mwenyekiti, alikumbusha kwamba Jengo la Klabu ya Yanga huitwa Ikulu na watu wanaofanya kazi Ikulu kwenyewe (State House), Mtaa wa Twiga ambao ndiko makao makuu ya Klabu ni Nembo ya Taifa, mwenge ulioko kwenye nembo ya Klabu ndiyo ambao hukimbizwa nchini kila mwaka na rangi zake ndiyo rangi za taifa, hivyo akiinunua Klabu, Wanachama wake watakuwa wamemuuzia Taifa hili, jambo ambalo ni ukoloni. Klabu inajiendesha kwa hasara na Wanachama wote wanaofikiri wanaweza kumiliki sehemu ya Klabu kwa miaka mitatu zaidi ya kujiendesha kwa hasara watafilisika kifedha na yeye na labda wengine wachache watamiliki Hazina ya Taifa.
Mwenyekiti, aliwakumbusha Wanachama kwamba historia ya Yanga si kama Klabu ya kawaida na kwamba katika kuwaigiza watu wengine wanavyo endesha mambo yao ni uhaini na matusi kwa kumbukumbu ya wale wote ambao wanaiona Yanga kama alama ya Uhuru.
- 7.4. Mwenyekiti, aliongeza kusema kwamba, chini ya Katiba ya 2010 ambayo TFF inapenda kuishinikiza kwa Yanga, yeye hataweza kuiendesha Yanga kwa kiwango cha nidhamu ambayo inatakiwa lakini wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa na Wanachama kwa kisingizio cha Katiba ya uchaguzi wa 2010 watairudisha Klabu kwenye aibu ya kuchapwa mabao 5 kwa 0, aibu iliyochukua miaka mitatu kuanza kuifuta machozi na bado deni ya moja na riba ya goli moja tunadaiwa. Hilo lote tulilipa na kwamba katika miaka minne iliyopita bado tuliinyima Simba kushiriki katika mashindano ya Kimataifa.
Kwa kutumia Katiba ya 2010, Yanga inarejea tena katika migongano kwani Mwenyekiti, hana nguvu ya kuwawajibisha wajumbe wa Kamati ya Utendaji. Na kwa vile Yanga imebaini kwamba uchaguzi unaweza kuendeshwa kwa amani, haraka na kwa gharama ndogo, Mwenyekiti, alisema kwamba sababu pekee iliyomfanya agombee nafasi hiyo ni kwa vile Klabu iko katika mchakato wa kihistoria na akapendekeza kwamba ajiuzulu nafasi hiyo Jumapili na Yanga ifanye uchaguzi na Wanachama wamchague Mwenyekiti mpya anayetaka kuiuza Klabu kama walivyofanya Simba, basi wafanye hivyo chini ya Mwenyekiti huyo mpya na siyo yeye.
- 7.5. Wanachama waliendelea na mdahalo huo lakini hawakutoa ufumbuzi wa moja kwa moja kwa sababu upande mmoja walipenda Mwenyekiti abaki na upande mwingine walikuwa wana kiri utamaduni wa kuendesha Klabu chini ya katiba ya mwaka 2010 itawarudisha kwenye machozi. Mwenyekiti, ilibidi awape Wanachama njia – aliwakumbusha Wanachama kwamba alikuwa na kiti katika jikoni ya Muafaka wa mwaka 2006 na iliyotoa Rasimu iliyofuata na kurudisha umoja wa Yangailiyopotea kwa sababu ya makundi ya YangaAsili, Yanga Kampuni na Yanga Academia. Rasimu ya 2006 ilikubali kwamba mali zilizopo, siku zote zitaendelea kuwa za Klabu, lakini Klabu inaweza kuikodisha timu na nembo kwa kampuni inayotaka kuwashirikisha Wanachama ikichukua asilimia 51 kwa kodi ya shilingi milioni 100,000,000/= kwa mwaka.
- 7.6. Kwa msingi huo, Mwenyekiti, alipendekeza kwamba akodishiwe timu, nembo yake na haki zote za Klabu kuhusu mpira kwa miaka 10 ambapo hasara yotea kampuni yake itabeba na Klabu ingepata asilimia 25 ya faida kama ikitokea na uwezo wake wa biashara ili hiyo alisema iwapo hilo lingekubalika, angeiinua timu hadi katika kiwango cha juu ambacho Wanachama wanakitaka bila mgogoro za Katiba ya elfu 2010, na kwamba angefanya juu chini kuhakikisha Klabu inakuwa na fedha na matunda yenye faida baada ya miaka 10 ambapo timu ingerudishwa tena mikononi wa Klabu - Mwenyekiti,alisema alikuwa akifanya hivyo si kwa njama ya kuifanya Yanga iwe mikononi mwa watu wachache bali kuhakikisha inaendelea kuwa mikononi mwa umma wa Wanannchi.
- 7.7. Mwenyekiti, alisema angeshirikiana na Bodi ya Wadhamini kuhakikisha Klabu inalindwa ambapo matawi na viongozi wake wanaendelea kuhamasishana kuwavuta watu kuwa Wanachama wa Yanga, yote haya ni kutekeleza nia ya waasisi wa Yanga waliotaka Klabu hiyo iwe ya wananchi na si ya wachache.
- 7.8. Pamoja na kwamba kulikuwa kuna Wanachama wanaotaka kuiuza Klabu, Mwenyekiti, alifupisha mdahalo na kuwaambia Wanachama kwa vile TFF imeonyesha chuki yake kwa Yanga, hilo litaleta matatizo kwani litawagawa Wanachama wa Klabu na hivyo kuifanya timu ifanye vibaya katika harakati za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu. Hata hivyo, Wanachama walimwelewa na kutambua jinsi ambavyo siku zote amesimama na ataendelea kusimama kupigania fahari ya Klabu.
- 7.9. Ilikubalika kwa pamoja kwamba kampuni ya Mwenyekiti,ikodishiwe timu, nembo yake na haki za Klabu kwenye mpira kwa miaka 10 na kwamba atabeba hasara yote itakayo patikana na faida kama ikipatikana asilimia 25% ilipwe kwenye Klabu ili Klabu iweze kujenga uwezo wa kusimamia timu yake baada ya miaka 10. Pia ilikubaliwa kuwepo na uwazi, baraza la Wadhamini wa Klabu litatoa Mkaguzi huru wa kupitia hesabu za kila mwaka ili Klabu isihujumiwe. Baraza la Wadhamini wa Klabu na Kampuni ya Mwenyekiti wafanye harakati za kuharakisha mkataba wa makubaliano uingizwe kwa mwandishi ili Mwenyekiti aweze kuanza mapambano na kuleta maendeleo kwa Yanga mara moja iwezekanavyo.
- 7.10. Mwenyekiti, aliwapa fursa Wadhamini kuwahakikishia kwamba watailinda Klabu katika mkataba husika, na Wadhamini hao watafanya kama walivyoombwa, na kama walivyoagizwa na Wanachama kwa uangalifu na uwazi kulingana na Imani waliyokuwa nayo wanachama kwao.
- 8. Baada ya kila kitu kukamilika Mwenyekiti, alitangaza kumalizika kwa mkutano huo kwa sala
Sala ya Kiislam ilisomwa.
Sala ya Kikristo ilisoma na.
- 9. Mkutano ulifungwa
……………………… ……………………….. 1,640
Yusuf Mehbub Manji Baraka Deusdecit
(Mwenyekiti,) (Kaimu Katibu Mkuu) Idadi ya Wanachama Waliokuwepo
CC: Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Young African Sports Club