Thursday, September 29, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SIMBA SPORTS CLUB
     DAR ES SALAAM
            29-6-2016

Klabu ya Simba inayo furaha kubwa ya kutangaza kumshukuru mlezi wake bwana Mohammed Dewji kwa kuanza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo.

Dewji maarufu kama MO tayari ameshaanza kulipia mishahara ya wachezaji,benchi la ufundi na Sekretarieti ya klabu na atafanya hivyo katika kipindi chote cha mpito kuelekea mabadiliko ya kimuundo ya klabu.

Mbali ya hayo mfanyabiashara huyo mkubwa barani Afrika atalipia kodi za nyasi bandia na gharama nyingine za uendeshaji wa klabu.

Uongozi wa Simba unamshukuru sana MO,ukizingatia klabu kwa sasa haina mdhamini na unaamini uwekezaji huo ni chachu ya kuwarejeshea furaha wanasimba na hatimae kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya msimu huu na misimu mingi ijayo.

Mwisho klabu inawaomba washabiki wake wajitokeze kwa wingi siku ya Jmosi ya Octoba Mosi pale uwanja wa Taifa,kuishangilia Timu yao itakapocheza mechi ya ligi dhidi ya Yanga.

Tunaamini mechi hiyo ni mwendelezo wa furaha kwa wanachama na washabiki wetu kote nchini.

Pia tuwaombe sana kukumbuka kununua tiketi kwa mawakala wa Selcom waliopo katika maeneo mbalimbali.
Ikumbukwe tiketi za mechi hii ni za kieletroniki.

Imetolewa na
HAJI S.MANARA.
MKUU WA HABARI
SIMBA SC

SIMBA NGUVU MOJA

Monday, September 19, 2016

NILICHOKIONA NA KUJIFUNZA KRC GENK.

1- MASHABIKI / WANACHAMA.

MASHABIKI WANAPENDA KWELI KWELI TIMU YAO NA WALA HUNA UNACHOWADANGANYA KUHUSU TIMU GENK YAO.

WANACHAMA WANA FAIDA KUBWA SANA KATIKA TIMU NA NAWEZA KUSEMA WAO NDIO WANACHANGIA KWA KIASI KIKUBWA MAPATO YA TIMU KWA MAANA WAO HAWAPO KWA AJILI YA TIMU IWAHUDUMIE WAPO ILI WAIHUDUMIE TIMU YAO.

KILA TAWI LA KRC GENK LINA KILA KITU KINACHOWAWEZWESHA KUSAIDIA TIMU YAO.

MATAWI YANA MABASI YAO MAALUM YA KUWASAFIRISHA POPOTE PALE TIMU YAO ITAKAPOCHEZA.

TIKETI ZA MSIMU ZINA FAIDA KUBWA KULIKO ZILE ZA KUUZWA KWA KILA MECHI.

2- WACHEZAJI .

SIKU YA MECHI AMBAYO TIMU INACHEZA NYUMBANI WACHEZAJI WANAKUJA KILA MMOJA AKITOKEA NYUMBANI KWAKE KWA MAANA KILA MCHEZAJI ANA GARI LAKE NA ATA SAMATTA PIA ANA BMW YAKE YANI MPYA KABISA HII NDIO AMEKUJA NAYO AKIWA PEKE YAKE NA KURUDI NAYO AKIWA PEKE YAKE YANI ANAENDESHA MWENYEWE .

SAMATTA NI MTU MUHIMU SANA KATIKA GENK NAWEZA KUSEMA YEYE NDIO ANAONGOZA KWA MASHABIKI WA GENK KUTAKA KUPIGA NAE PICHA HUKU KILA MMOJA AKIOMBA KITU CHOCHOTE KUTOKA KWAKE.

MASHABIKI WENGINE WANAOMBA JAPO WAPEWE NDALA NA SAMATTA ILI WAKAWEKE NDANI IWE KUMBUKUMBU.

JEZI YA SAMATTA KUIPATA UWANJANI INABIDI UWEKE ODA NDIO AKUVULIE AKUPE.

3-BIASHARA MAENEO YA UWANJA.

KILA UTAKACHOKIONA KINAUZWA MAENEO YA UWANJANI BASI UJUE TIMU ISHALIPWA YANI UKIFANYA BIASHARA ATA YA ICE CREAM INABIDI ULIPIE CLUB KINYUME CHAKE MTAELEZANA MBELENI.

HAPA NIMEPATA SOMO YA KUWA NA UWANJA TIMU HAIWEZI KULIA NJAA.

4-TIKETI ZA UMEME.

KAMA HUNA TIKETI HUWEZI KUINGIA NDANI KWA MAANA HUWEZI KUFUNGUA MLANGO ILI UPATE KUPITA.

HII INASAIDIA KULINDA MAPATO YA TIMU NA PIA USALAMA WA RAIA WAWAPO UWANJANI.

UKIWA NA TIKETI ATA UFIKE SAA NGAPI UWANJANI KITI CHAKO UTAKIKUTA TU.

5-AMASA YA MASHABIKI.

MASHABIKI WAO NI MOJA KATIKA VYANZO VYA USHINDI MAANA SAPOTI YAO NI KUBWA SANA PALE UWANJANI.

NB : SIMBA NA YANGA HAYA MAMBO YANAWEZEKANA IKIWA TU VIONGOZI TUTAKAOWAPA TIMU NI WALE WENYE DAMU YA TIMU ASAA.

TUKIENDELEA KUWAPA TIMU WANASIASA AMBAO HAWAJUI NINI MAANA YA MPIRA WALA HAWAJUI TIMU ILIANZAJE TUTAENDELA KUZIMIA VIWANJANI HUKU TIMU ZIKIENDELEA KUWA OMBAOMBA .

TUNAKOSEA KUWAPA TIMU WAFANYABIASHARA AMBAO WANAKUJA KWA AJILI YA KUONGEZA VIPATO VYAO.

TUWAPE TIMU WENYE ASILI YA TIMU YAO TUACHANE NA WAPIGAJI.

NDIO MAISHA LAKINI.

Thursday, September 8, 2016

DANNY LYANGA HUYOO APAA OMAN


Sheila Ally, Dar

 STRAIKA wa Simba, Danny Lyaga jana aliondoka kwenda Oman kwa ajili ya kufanya majaribio ya wiki mbili na timu ya Oman Club inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza.

Lyanga amechukuwa uamuzi huo baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha Joseph Omog ambapo tangu ligi ianze hajacheza mechi hata moja na hivyo kumuweka katika wakati mgumu hasa kulinda kipaji chake.

Rais wa Simba, Evans Aveva amethibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo na kwamba endapo atafuzu basi wapo tayari kufanya biashara.

"Tumemruhusu kwenda huko na akifanikiwa na kama wao Oman Club watamuhitaji basi tutawasikiliza ofa yao ya kumnunua nasi tutamuuza pasipo tatizo, maana kila kitu ni mazungumzo," alisema Aveva.

Lyanga hapati nafasi kutokana na ushindani mkubwa toka kwa Laudit Mavugo, Ibrahim Ajibu na Fredrick Blagnon.

Saturday, September 3, 2016

POLISI DODOMA KUWAPIMA SIMBA SC LEO



Na Abdallah Mohamed, Dodoma


Timu ya Polisi ya mkoani hapa leo itajitupa uwanja wa Jamhuri kujipoima dhidi ya Simba SC katika mechi inayotarajiwa kuwa ya kusisimua.
Ikiwa na mshambuliaji wake matata Fredrick Blagnon,Simba itajiuliza kwa mara nyingine leo baada ya kupata sare na JKT RUVU katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara wiki iliyopita.

ENGLAND YAINGIA MCHECHETO UTEUZI WA ALLARDYCE

Sam Allardyce ameteua kikosi chake ya Timu ya Taifa ya England kwa mara ya kwanza kabisa kitakachowavaa Slovakia kesho Jumapili, na tayari watu wengi wameonekana kutofurahishwa.
Meneja huyo ameamua kubaki na wachezaji wengi ambao walionesha kiwango kibovu katika michuano ya Euro, na hali hiyo imewaacha watu wengi wakijiuliza kama kweli Allardyce ataonesha utofauti wowote dhidi ya Hodgson kwenye timu hiyo.
Baadhi ya wachezaji hao ni:
Hart, Walker, Cahill, Stones, Rose, Dier, Henderson, Lallana, Rooney, Sterling, Kane.
Bila shaka John Stones inaonekana kabisa atapata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza baada ya kuwa na kwenye kiwango bora kabisa msimu uliopita na kufanikiwa kijiunga na Manchester City.
Hata hivyo wengi wanajiuliza juu ya uwepo wa wachezaji kama Henderson na Kane kutokana na kiwango chao kisichoridhisha kwenye Michuano ya Euro.
Drinkwater ameachwa tena
Washabiki wengi wanajiuliza inakuaje tena mchezaji kama Danny Drinkwater anaachwa halafu Henderson anachukuliwa.
Ni ukweli ulio wazi kwamba msimu uliopita Drinkwater alicheza kwenye kiwango cha hali ya juu mno bila kusahau kwenye mechi hizi za awali za msimu huu licha ya kutokuwepo kwa pacha wake N’Golo Kante ambaye ametimkia Chelsea.